Aliyasema hayo baada ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Istiqlal jijini Jakarta, Indonesia, alipohudhuria mkutano wa 19 wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC).
Alisema: “Leo hii, ni wajibu wetu wa Kiislamu kusimama pamoja kwa umoja na tusiruhusu ujeuri wa kimataifa kuendeleza mauaji makubwa zaidi ya kimbari katika historia."
“Leo, watu wa Gaza, wakiwemo watoto, wanawake na wagonjwa, wanatarajia tuwe nao bega kwa bega. Wanataka tuwe sauti ya wanyonge na tusiwaache peke yao katika siku hizi ngumu.”
Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, lakini hadi sasa haijafanikiwa kutimiza malengo yake iliyoainisha, licha ya kuwaua angalau Wapalestina 53,010, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 119,998.
Utawala huo ulilazimika kukubali masharti ya muda mrefu ya mazungumzo yaliyowekwa na kundi la Muqawama la Hamas chini ya usitishaji mapigano wa Gaza ulioanza Januari 19. Hata hivyo, Israel ilikiuka makubaliano hayo tarehe 2 Machi kwa kukata misaada ya kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza. Zaidi ya wiki mbili baadaye, utawala huo uliendelea tena na mashambulizi makali na kurudisha wanajeshi katika eneo hilo linalozingirwa.
Qalibaf amesema kuwa Israel haijaruhusu hata dawa kuwafikia wagonjwa walioko Gaza, ambako watoto wa Kiislamu wanaishi kwa hofu ya kuuawa si tu kwa mashambulizi ya Israel, bali pia kwa njaa, kiu na magonjwa.
Leo hii, aliongeza, Waislamu duniani na watu wanaopenda haki wanaitikia wito wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Khomeini, wa kupinga “uvimbe wa saratani” unaoitwa Israel.
Pia alisisitiza kuwa watu wa Iran wamekuwa daima wakiiunga mkono Palestina na hawatakata tamaa kufanya hivyo licha ya shinikizo na vitisho.
Your Comment